"

SURA YA II: KUJITAMBULISHA

9 Lesson 3: Lugha, Nchi, na Uraia

Performance Objectives

By the end of this lesson, the learner will be able to;
  • state the language they speak, their nationality, and their country of origin.
  • ask and answer questions about their nationality, country of origin, and languages they speak.

Msamiati

LUGHA NCHI URAIA
Kichina Uchina Mchina
Kiswahili Kenya/Uganda/Tanzania Mkenya/Mganda/Mtanzania
Kiingereza Uingereza Mwingereza
Kijapani Ujapani Mjapani
Kireno Ureno Mreno
Kifaransa Ufaransa Mfaransa
Kiitaliano Uitaliano Mwitaliano
Kihispania Uhispania Mhispania
Kiganda Uganda Mganda
Kirusi Urusi Mrusi
Kiyahudi Uyahudi Myahudi
Kikorea Korea Mkorea
Kilingala Demokrasia ya Kongo Mkongo
Kijerumani Ujerumani Mjerumani
Kiingereza Marekani Mmarekani
Kiarabu Mwarabu

N/B: All languages take the prefix ki- when translated to  Swahili language. The prefix M-, on the other hand, is used to mark nouns of nationality, like in the phrases Mimi ni Mmarekani and Mimi ni Mtanzania. Look at the following chart that shows the shared root of words that refer to country, language, and citizenship. All citizenship will have an m- prefix for singular and wa- for plural

Unasema/Ongea/Zungumza

  1. Unasema lugha gani?
  • Ninasema Kiswahili, Kiingereza na Kikorea kidogo

2. Unazungumza lugha gani?

  • Ninazungumza Kiitaliano

3. Unaongea lugha gani?

  • Ninaongea Kiingereza, Kiswahili na Kichina

Mfano

  1. Unasema lugha gani?
  • Ninasema Kiswahili.

2. Unatoka nchi gani?

  • Ninatoka Marekani

3. Uraia wako ni nini?

  • Mimi ni mmarekani.

Zoezi la 1: Fill in the table with the correct language and citizenship.

Zoezi la 2: Kusikiliza

Listen to your instructor saying a few things about themselves. Listen for information about their name, occupation, and where they’re from.

Now answer these questions.

  1. Jina lake ni nani?
  2. Mwalimu anatoka Tanzania? (negate)
  3. Uraia wa Mwalimu ni gani?
  4. Yeye ni mwanafunzi?
  5. Mwalimu anafundisha wapi?
  6. Mwalimu anafundisha nini?
  7. Mwalimu anasema lugha gani?
  8. Mwalimu anasema Kichina na kijapani pia. Ni kweli au Si kweli?

Zoezi la 3: Kusilikiza na kuandika

Listen to some of the students in the Swahili class introduce themselves.  Mark the language(s) that each of them speaks. Then, answer questions about each speaker.

        As you listen, take notes in the table below the name of each speaker and the language they speak.
After listening, answer these questions:
       

       

Zoezi la 4: Soma mazungumzo  kisha ujibu maswali haya

Mazungumzo 1: Uraia, Nchi, na Lugha

Patel:Hujambo?

Rashida:Sijambo!

Patel: Habari za asubuhi?

Rashida: Nzuri sana.

Patel: Jina langu ni Patel, mimi ni Mhindi, ninatoka India. Ninaongea Kihindi kingi na Kiingereza kidogo. Je, wewe unaitwa nani?, unatoka wapi? na unazungumza lugha gani?

Rashida: Mimi ninaitwa Rashida, mimi ni raia wa Tanzania, kwa hivyo mimi ni Mtanzania. Ninazungumza Kiswahili kingi na Kiigereza kidogo.

Patel: Ninafuraha kukutana na wewe.

Rashida: Mimi pia.

Patel: Haya, kwaheri.

Rashida: Kwaheri ya kuonana

Maswali

  1. Patel anatoka wapi?
  2. Patel anazungumza lugha gani?
  3. Patel anasema Kiswahili?
  4. Uraia wa Rashida ni gani?
  5. Rashida anasema lugha gani?

Zoezi la 5: Kuandika

Jibu maswali haya

  1. Jina lako ni nani?
  2. Unatoka nchi gani?
  3. Unasema lugha gani
  4. Wewe ni mzaliwa wa nchi gani?
  5. Uraia wako ni gani?

License

Icon for the Creative Commons Attribution 4.0 International License

Elementary Swahili I Copyright © by Gorrety Wawire is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License, except where otherwise noted.