SURA YA V: SHUGHULI ZA KILA SIKU
21 Lesson 2: Ratiba Yangu
Performance Objectives
- describe what you do regularly
- master telling time
- give their daily schedule using the habitual hu-
Msamiati wa shughuli za kila siku
Kiswahili | English | Kiswahili | English |
Kuamka | To wake up | Kuoga | To shower |
Kulala | To sleep | Kuimba | To sing |
Kucheza | To play | Kula chakula cha asubuhi | To eat breakfast |
Kutazama televisheni | To watch TV | Kula chakula cha jioni | To eat dinner |
Kusikiliza muziki | To listen to music | Kutembeza mbwa | To walk the dog |
Kulala | To sleep | Kusafisha vyombo | To clean dishes |
Kuenda shuleni | To go to school | Kupika chakula | To cook food |
Kusoma | To read/to study | Kupiga huva | To vacuum |
Kupiga mwaski | To brush teeth | Kuosha bafu na choo | To clean the toilet and the bathroom |
Kunawa uso | To wash the face | Kucheza dansi | To dance |
Kucheza muziki | To play music | Kusafiri | To travel |
Kula chakula cha mchana | To eat lunch | Kwenda shuleni | To go to school |
Kwenda kazini | To go to work | Kwenda darasani | To go to class |
Kulima shamba | To till the land | Kufagia | To sweep |
Kukama ng’ombe | To milk a cow | Kupiga deki | To mop |
Kukata nyasi | To cut grass/mow the lawn | Kutandika kitanda | Make bed |
Zoezi la 1: Msamiati
These activities are common among family and friends in East Africa. In groups of 3, compare and contrast and mark activities that are shared between East Africans and your own culture.
Watu hufanya nini? | Mwanafunzi 1 | Mwanafunzi 2 | Mwanafunzi 3 |
Kusikiliza muziki | |||
Kukama ng’ombe | |||
Kupika chakula | |||
Kukata nyasi | |||
Kwenda kazini | |||
Kula chakula cha asubuhi | |||
Kwenda shuleni | |||
Kufagia | |||
Kucheza dansi | |||
Kulima shamba | |||
Kuoga | |||
Kulala | |||
Kuosha bafu na choo | |||
Kutandika kitanda | |||
Kupiga deki |
Discuss the similarities and differences between your own cultures and the East African culture.
Zoezi la 2: Kusoma
Monolojia 1: Ratiba ya Juma
Mimi ni Amina. Mimi huamka saa moja kamili asubuhi. Baada ya kuamka mimi huoga kisha hupiga mswaki. Baada ya kupiga mswaki mimi huvaa nguo kisha hupika chakula cha asubuhi. Mimi hula chakula cha asubuhi saa mbili kamili. Mimi huenda darasa la Kiswahili saa nne na dakika kumi asubuhi hadi saa tano kamili mchana. Baada ya darasa la Kiswahili mimi huenda darasa la Kemia kisha mimi hula chakula cha mchana saa sita kamili mchana. Kisha mimi huenda nyumbani.
Maswali (Write all times in numbers)
- Jina lake ni nani?
- Amina huamka saa ngapi?
- Amina hufanya nini baada ya kuamka?
- Yeye hufanya nini kabla ya kupika chakula cha asubuhi?
- Amina huenda darasa la Kiswahili saa ngapi?
- Darasa la Kiswahili huisha saa ngapi?
- Yeye hula chakula cha mchana saa ngapi?
Zoezi la 3: Ratiba ya Imani ya Asubuhi (KUSIKILIZA)
Write a summary of Imani’s schedule below
Zoezi la 4: Kueleza ratiba yako
- You and your friend are trying to find a time to meet on Monday to work on a class project. You decide to send her a quick summary of your Monday schedule to help coordinate.
Zoezi la 5: Andika sentensi kueleza ratiba ya Jamila
Based on the pictures provided, write six sentences to describe Jamila’s evening schedule.
Photo by Greg Pappas on Unsplash
Photo by Kevin McCutcheon on Unsplash
Photo by Kevin McCutcheon on Unsplash
Photo by Diana Polekhina on Unsplash
Photo by Jingxi Lau on Unsplash
Photo by Alexunder Hess on Unsplash
Zoezi la 6: Kusoma
Soma kuhusu ratiba ya Malaika kisha ujibu maswali. (Malaika describes her schedule to Jamila and Amina. They are trying to figure out a time to meet for brunch, lunch, or dinner, but Malaika’s day seems to be busy.
Hamjambo rafiki,
Mimi huwana kazi na madarasa mengi kila siku. Mimi huamka saa mbili na nusu asubuhi. Baada ya kuamka, mimi huoga, huvaa nguo, na hupiga mswaki. Kisha mimi hupika chakula cha mchana. Mimi hupakia na kubeba chakula cha mchana. Mimi huwa sili chakula cha asubuhi. Mimi huenda darasani saa tatu kamili asubuhi hadi saa tatu na dakika hamsini mchana. Baada ya darasa mimi huenda kazini kutoka saa nne kamili mchana hadi saa sita na nusu mchana. Baada ya kazi mimi hula chakula cha mchana kisha huenda darasa la Biashara saa saba kamili hadi saa nane na dakika ishirini. Baada ya darasa mimi hupumzika kisha hufanya mazoezi kutoka saa tisa na nusu hadi saa kumi na nusu. Mimi huenda darasa la Anthropolojia saa kumi na moja kamili hadi saa kumi na mbili na dakika ishirini. Mimi huenda nyumbani saa kumi na mbili na nusu.
Asanteni,
Malaika
Maswali
- Malaika huamka saa ngapi?
- Malaika hufanya nini baada ya kuamka?
- Malaika huenda darasa la kwanza saa ngapi?
- Malaika huenda darasa la mwisho saa ngapi?
- Malaika huanza kazi saa ngapi?
- Malaika hufanya nini kabla ya Kwenda darasa la Athropolojia?
- Malaika hufanya nini baada ya kupika chakula cha mchana?
- Malaika hula chakula cha asubuhi saa ngapi?
- Malaika huenda nyumbani saa ngapi?
- Malaika hupumzika kwa muda gani?
Zoezi la 7: Kuzungumza Ratiba ya Maria
Your friend Maria called you and left a voicemail about an excursion they have over the weekend. They would like to know your schedule so they can plan activities and meals for the excursion. Record a voice note giving your schedule.