"

SURA YA V: SHUGHULI ZA KILA SIKU

23 Lesson 4: Shughuli za Wikiendi 

Performance Objectives

By the end of this lesson, the learner will be able to

  • describe their weekend plans, detailing the times they do different activities

 Grammar: Future Tense and Its Negation

An affirmative future tense verb in Swahili is:

Subject Prefix + Tense Marker (-ta-) + Verb Stem + Final Vowel (-a)

Person Subject Prefix Example
Mimi Ni Nitasoma/I will read
Wewe U Utasoma/You will read
Yeye A Atasoma/He/She will read
Sisi Tu Tutasoma/ We will read
Nyinyi M Mtasoma/ You all will read
Wao Wa Watasoma/ They will read

Mfano; Nitasoma

   Ni                             ta                   som                    a

Subject Prefix + Tense Marker + Verb Stem + Final Vowel (-a)

The tense marker for the future tense is -ta-. It indicates that the action will happen in the future. The verb stem is the root of the verb (e.g., from “kusoma” (to read), the stem is “-soma”). The final vowel for most Swahili verbs in the affirmative is -a.

Negation of Present Tense

Negating the future tense in Swahili involves a few changes. The affirmative subject prefixes are replaced by a negative subject prefix. The future tense marker -ta- does not change. The final vowel does not change either.

Negative Subject Prefix + Verb Stem + Final Vowel (-a)

Person Subject Prefix Example
Mimi Si Sitasoma/I will not read
Wewe Hu Hutasoma/You will not  read
Yeye Ha Hatasoma/He/She will not read
Sisi Hatu Hatutasoma/ We will not read
Nyinyi Ham Hamtasoma/ You all will not read
Wao Hawa Hawatasoma/they will not read

Zoezi la 1: Future tense -ta

Zoezi la 2: Wewe utafanya nini wikendi?

Juma: Hujambo  Bahati?

Bahati: Sijambo na wewe je?

Juma: Mimi pia sijambo.

Bahati: Utafanya nini wikendi hii?

Juma: Mimi nitafanya vitu vingi wikendi hii.

Bahati: Utaamka saa ngapi?

Juma: Mimi nitaamka saa nne asubuhi. Ninapenda kulala wikendi. Na wewe je?

Bahati: Mimi nitaamka saa kumi na mbili asubuhi.

Juma: Kwa nini?

Bahati: Nitakimbia na kufanya mazoezi. Utafanya nini baada ya kuamka?

Juma: Nitasafisha chumba kisha nitakula chakula cha asubuhi. Wewe utafanya nini baada ya kukimbia?

Bahati: Nitafua nguo kisha nitaenda dukani.

Juma: Nitaenda dukani pia saa sita mchana na baadaye nitafanya kazi ya nyumbani

Bahati: Mimi nitapika chakula cha mchana kisha nitazungumza na wazazi wangu kwa simu. Utafanya nini Jumamosi jioni?

Juma: Nitatazama filamu hadi saa nne usiku kisha nitalala. Na wewe je?

Bahati: Nitaenda kwa rafiki yangu saa moja kamili usiku. Mimi nitalala usiku wa manane wikendi kwa sababu sitaenda shuleni.Wewe hufanya nini Jumapili?

Juma: Mimi huenda kanisani asubuhi kisha mimi hupumzika mchana. Na wewe je?

Bahati: Mimi huenda kanisani asubuhi pia kisha mimi hufanya kazi ya nyumbani.

Asante, na wikendi njema.

Juma: Wikendi njema pia

Answer the following true or false questions.

  1. Juma hulala wikendi yote? Kweli au si kweli
  2. Bahati huamka mapema wikendi. Kweli au si kweli
  3. Juma na Bahati wataenda sokoni wikendi. Kweli au si kweli
  4. Bahati atafanya kazi ya nyumbani Jumamosi. Kweli au si kweli
  5. Wikendi, Juma hufanya vitu vingi zaidi kuliko Bahati. Kweli au si kweli
  6. Juma na Bahati huenda kanisani Jumamosi. Kweli au si kweli

Zoezi la 3: Kuzungumza

Your classmate would like you to join them for a friend’s birthday party. You look at your schedule, and it looks a bit tight. Leave her a voice message describing your Saturday schedule and politely decline the invitation.

Zoezi la 4: Siku moja katika Maisha yangu

Pick either your favorite or, worse, busiest or slowest day of the week and create a 1-2 video presentation with pictures describing your routine for that day from morning to evening, including the times that you do each activity. Share the recording with the class for peer evaluation.

 

License

Icon for the Creative Commons Attribution 4.0 International License

Elementary Swahili I Copyright © by Gorrety Wawire is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License, except where otherwise noted.