SURA YA VII: VYAKULA NA MAPISHI
31 Lesson 2: Vyakula Vya Afrika Mashariki
Performance Objectives
By the end of this module, students will be able to;
- learn about common foods (products) and mealtime practices in East Africa.
- engage in conversations, understand and interpret spoken Swahili, and present information about their food preferences.
- recognize and identify at least four common East African foods when I hear their names
Msamiati
VYAKULA VYA AFRIKA MASHARIKI
Chakula cha Asubuhi
· Chai kwa mkate na mayai · Chai/kahawa kwa Maandazi · Chai/uji kwa viazi vitamu · Chai kwa samosa · Maji ya matunda kwa samosa/mandazi/ · Chai kwa chapati · Chai kwa mkate na njugu |
Chakula cha mchana
· Ugali kwa nyama na sukumawiki na mchicha · Wali na maharagwe · Pilau na kachumbari · Chapati kwa maharagwe · Ugali kwa nyama ya kuku na sukuma wiki · Biriyani · Nyama choma (mbuzi) · Ugali na sukumawiki · Wali kwa nyama ya Ng’ombe na kajebi |
Chakula cha jioni
· Ugali kwa nyama na sukumawiki na mchicha · Wali na maharagwe · Pilau na kachumbari · Chapati kwa maharagwe · Ugali kwa nyama ya kuku na sukuma wiki · Biriyani · Nyama choma (mbuzi) · Ugali na sukumawiki · Wali kwa nyama ya Ng’ombe na kajebi |
Vinywaji
· Maji · Chai · Kahawa · Uji · Maji ya matunda · Maji ya Nazi |
Zoezi la 1: Msamiati
After learning about East African food in class, your teacher will present you with a jar of pictures of different East African foods. The pictures will be shuffled, then you will pick one and using the vocabulary learned, you will describe the food that you picked and explain to the class whether you like it or not.
Zoezi la 2: Watu hula nini?
The table above represents foods and drinks that are common for breakfast, lunch, and dinner among families and friends in East African communities. In groups of 3, compare and contrast and write food and drinks that are common in your culture and shared between East Africans and your own culture. Note down the similarities and provide your list of foods for breakfast, lunch, and dinner if there are no similarities. Fill in the information in the table below.
Watu hula nini? | Mwanafunzi 1 | Mwanafunzi 2 | Mwanafunzi 3 |
Chakula cha asubuhi | |||
Chakula cha Mchana | |||
Chakula cha jioni | |||
Vinywaji |
Zoezi la 3: Kuzungumza
Maswali: Unapenda kula nini?
Based on the foods and drinks listed above, answer the following questions, stating what you like to eat and drink
- Wewe unapenda kula nini kwa chakula cha asubuhi?
- Wewe hula chakula cha asubuhi saa ngapi?
- Wewe unapenda kula nini kwa chakula cha mchana?
- Wewe hula chakula cha mchana saa ngapi?
- Wewe unapenda kula nini kwa chakula cha jioni?
- Wewe hula chakula cha jioni saa ngapi?
- Unapenda vinywaji gani?
Zoezi la 4: Kusoma
Soma mazungumzo kati ya Simba na Bahati
Simba: Hujambo Bahati?
Bahati: Sijambo Simba. Na wewe je?
Simba: Mimi pia sijambo. Uhali gani?
Bahati: Nzuri sana. Unaenda wapi?
Simba: Ninaenda kula chakula cha mchana.
Bahati: Ni mapema sana?
Simba: Mimi hula chakula cha mchana saa sita kamili kwa sababu huwa sili chakula cha asubuhi. Wewe hula chakula cha mchana saa ngapi?
Bahati: Mimi hula chakula cha mchana saa 2:00.
Simba: Kwa nini?
Bahati: Kwa sababu mimi hula chakula cha asubuhi saa tano na nusu asubuhi. Wewe hula nini kwa chakula cha mchana?
Simba: Mimi hula wali, nyama ya kuku, kachumbari, saladi, na maji. Wewe hula nini kwa chakula cha mchana?
Bahati: Mimi hula Baga ya nyama ya ng’ombe na soda. Wewe hula chakula cha jioni saa ngapi?
Simba: Mimi hula chakula cha jioni saa 6:00 jioni. Na wewe je?
Bahati: Mimi hula chakula cha jioni 9:30 usiku. Wewe hula nini kwa chakula cha jioni?
Simba: Mimi hula ugali kwa nyama ya ng’ombe na sikuma wiki. na wewe je?
Bahati: Mimi hula pizza na saladi. Sawa sawa
Simba: Mimi ninaenda kula tutaonana baadaye.
Bahati: Kwaheri, tutaonana baadaye.
Zoezi la 5: Kuzungumza