"

SURA YA II: KUJITAMBULISHA

11 Lesson 5: Kusoma wapi

Performance Objectives

By the end of this lesson, learners will be able to;
  • talk about where they go to school and what they study
  • identify and name common school subjects in Swahili.

MSAMIATI

Kiswahili Kiingereza
chuo two-year college
chuo kikuu University
-soma Study
katika At
-fundisha Teach

Mazungumzo 1: Unasoma wapi

Mwalimu: Unasoma wapi?

Mwanafunzi: Ninasoma katika chuo kikuu cha Kenyatta. Na wewe je?

Mwalimu: Mimi ninafundisha katika chuo kikuu cha California Berkeley.

Mazungumzo 2: Two students meet during the Boren Award scholarship abroad. They introduce each other.

Issa:                 Jina langu ni Issa. Jina lako ni nani?

Mfalme:          Ninaitwa mfalme. Unasoma wapi?

Issa:                 Ninasoma katika chuo kikuu cha Illinois Urbana, Champaign. Unasoma wapi?

Mfalme:          Ninasoma katika chuo kikuu cha Baylor.  Mimi ni mwanafunzi wa Kiswahili.

Issa:                 Mimi ni Mwanafunzi wa Kiswahili pia. Nimefurahi kukufahamu Mfalme.

Mfalme:          Nimefurahi kukufahamu pia. Tutaonana baadaye

Issa:                 Tutaonana baadaye

Zoezi la 1: Unasoma wapi?

  1. Mfalme anasoma wapi?
  2. Issa anasoma wapi?

Mazungumzo 3: Mfalme meets Juma at the market in Tanzania

Mfalme: Hujambo Mfalme

Juma: Sijambo, na wewe je?

Mfalme: Mimi pia sijambo. Habari za mchana?

Juma: Nzuri sana. Habari za masomo?

Mfalme: Nzuri sana. Unasoma wapi Juma?

Juma: Mimi ninasoma katika chuo kikuu cha Dar Es Salaam.

Mfalme: Mimi pia. Ninaenda nyumbani. Tutaongea baadaye.

Juma: Sawa, kwaheri. Tutaongea baadaye.

Zoezi la 2: Scenario

One morning, you are on your way to Kiswahili class and see your friend(s) with a student you don’t know. Greet your friend(s) and ask about the new student. Make sure to find out who they are, where they are from, where they study, and any other relevant details.

Zoezi la 3: Listen to Maria introducing herself to her classmates.

Zoezi la 4: After listening to Maria answer the following questions.

Zoezi la 5: Kuzungumza

You are both new students at the University of Dar es Salaam and meet in the morning on your way to class. Using the phrases and vocabulary you have learned so far, greet each other and ask questions to get to know your peer better. Find out information such as their name, where they are from, what they are studying, and any other details you find interesting.

License

Icon for the Creative Commons Attribution 4.0 International License

Elementary Swahili I Copyright © by Gorrety Wawire is licensed under a Creative Commons Attribution 4.0 International License, except where otherwise noted.